WAISLAM WA DHEHEBU LA SHIA JIJINI DAR WAADHIMISHA SIKU YA ASHURA KUKUMBUKA KIFO CHA MJUKUU WA MTUME MOHAMMED (S.A.W
Pichani
Juu na Chini Waumini wa dhehebu la Shia wakiwasili na kukusanyika
katika eneo la makaburi ya Washia Kisutu jijini Dar es Salaam
wakijiandaa kuanza maandamano ya kuadhimisha siku ya Ashura kukumbuka
kifo cha Mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) Imam Hussein yaliyofanyika
jana.
Mwenyekiti
wa Msikiti wa Jamaat Shia Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa
waandishi wa habari amesema katika kuadhimisha siku hii Waislam wa
dhehebu la Shia watafanya matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi
katika msikiti mkuu wa Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo
ndani yake kutakuwa kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za
maombolezo tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi
kujipa uhai kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa
watu wake na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya
wenzake.
Imamu
wa Msikiti wa Imam Ali wa Magomeni Mapipa Msabaha Shaaban Ali Mapinga
akizungumza na waandishi wa habari amesema siku hii ni siku ya kukumbuka
na kuadhimisha miaka 1473 ambapo katika nchi ya Iraq kwenye mji wa
Karbala aliuwawa mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) aliyekuwa akijulikana
kwa jina la Imam Hussein Bin Ali Bin Abutwalib.
Amesema
katika nyakati hizo alitokea mtawala dhalim aliyekuwa akitetea dhulma
na kukiuka haki za binadamu kitendo ambacho mjukuu wa Mtume Imam Hussein
hakukubaliana nacho na kuunda jeshi lake dogo kutetea haki na kupinga
Batili.
Kwakuwa
Imam Hussein alikuwa na dhamana ya kutetea haki alikataa kuwa chini ya
mtawala huo ndipo alipotumiwa jeshi la watu kama 30,000 naye akiwa na
jeshi la watu 72 walipambana katika mji huo na mjukuu wa Mtume aliuwawa
kifo cha kikatili cha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
Kwa
Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum
amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu
tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha
kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi.
Amesema
kifo cha Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku
ambayo haki ilizimwa na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka
batil isimame , kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.
Aidha
Sheikh Salum amesema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam
wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni
mtetezi wa haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba
kutetea haki na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha
ya leo, kutetea wanyonge, kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna
yoyote ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.
Waumini
hao wakiwa wamejipanga tayari kuanza maadamano kutoka makaburi ya
Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia.
Pichani
juu na chini msafara wa waumini wa Shia umeanza.
Hisia
na Majonzi vilionekana.
Ni
jambo jema watoto kujua dini mapema, kama inavyoonekana pichani mtoto
akiwa ameambatana na mzazi wake katika maandamano ya siku ya Ashura.
Bango
lenye Ujumbe maalum wa siku ya Ashura.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment