TAYANA AFUNGUKIA SKENDO YAKUFUMWA NA MAKAMUA JENZI!!!

WIKI hii tunaye mwanadada Tayana Amri, ni mtangazaji lakini kwa sasa anafanya kazi ya U-MC katika lile Shindano la Tikisa na mlezi wa washiriki wa Shindano la Epiq Bongo Star Search. Wiki hii naye anajibu na kufafanua juu ya maswali ambayo mmemuuliza.

Big up!
Habari dada Tayana kwa kweli nafurahi kuwa na madada kama wewe, wewe ni kioo cha jamii, kazana dada na Mungu akubariki. Kelvin Mwaibula, Dar, 0713644447
TAYANA: Asante sana Kelvin, ubarikiwe pia.
Ameolewa?
Tayana nakuzimia sana uzuri wako na sauti yako kunako tasnia ya utangazaji Bongo, je umeolewa au una mchumba? Salim Liundi, Dar, 0658110395
TAYANA: Hahaha! Mimi ni mama wa watoto wawili.
Ushauri kwa wanawake wenzake
Unajituma sana kufanya kazi mbalimbali, je unatoa ujumbe gani kwa wanawake wenzako? Elia, Iringa, 0718085308
TAYANA: Ninawaambia kuwa uchakarikaji ni muhimu sana kwani maisha yamekuwa magumu.

Kabila lake
Hongera sana dada Tayana kwa kipaji chako, mimi napenda kuwa kama wewe lakini sina wa kunipa msaada, je wewe ni kabila gani? Anna Masemba, Dar, 0657625590
TAYANA: Asante sana, mimi ni mchanganyiko wa Mhaya na Mrusi, nitachukua namba yako nikutafute.

Umri wake
Dada Tayana nakukubali kwa kazi zako, nataka kujua una miaka mingapi, umezaliwa wapi? Ramadhani Hamisi, Tanga, 0717236195
TAYANA: Asante, huwa sipendi kutangaza umri wangu ila nimezaliwa Tukuyu, Mbeya.

Ufagio
Una muonekano mzuri, una sauti nzuri na unajiamini, kubwa zaidi hauna skendo za hivyo. Cassian, 0655202202
TAYANA: Asante sana, ubarikiwe.

Vita na wanaume wakware
Kuna wanaume wanaangalia nani kioo katika jamii wa kumchezea na kumuacha, je wewe umejiandaa vipi? Maka, Dar, 0712053834
TAYANA: Niko kwenye fani hii muda mrefu kwa hiyo ikikutokea unajifunza maisha ni shule tunajifunza kila siku.

Mafanikio yake
Vipi kuhusu mafanikio yako? France Lowassa, Arusha, 0654998984
TAYANA: Shukrani, mimi nawashukuru sana wote walionifundisha kazi hii na kwa kweli mafanikio ninayaona.

Hajaolewa ila ana watoto
Tayana umeolewa na una watoto wangapi? A2, Dar, 0756606012
TAYANA: Sijaolewa ila nina watoto wawili, Tamia miaka 12, na Russell miaka 4.

Mipango ya baadaye
Je, Tayana una mipango gani hapo baadaye? Msomaji, 0776831029
TAYANA: Mungu akijalia biashara zangu zikizidi kukua, nawatengenezea watoto wangu maisha bora pia nataka nirudi shule.

Idadi ya ‘alioduu’ nao
Nataka kujua ‘umeduu’ na mastaa wangapi mpaka sasa? Shabani Dacourt, Dar, 0714520163
TAYANA: Looo! Ingekuwa nimeduu na mastaa basi skendo zingeonekana, mambo mengine ni aibu mimi ni mtu mzima na ni mama.

Huyu anaomba undugu
Mimi naomba uwe dada yangu wa kujitolea tena naomba dada Tayana unisaidie nitoke kimaisha. Junioh, 0716804249
TAYANA: Nitakutafuta ndugu yangu.

Kuhusu kutoka na Makamua
Nakukubali sana Tayana, je ni kweli unaduu na Makamua na mlishafumwa sana Zenji mkila bata? King, 0719137366
TAYANA: Hapana ulikuwa ni uzushi tulikuwa fiesta Zanzibar na tulikuwa tunaogelea siyo peke yetu kulikuwa na watu wengine kibao.

Comments