
JOHN MAGANGA enzi za uhai wake.

TASNIA ya filamu nchini Tanzania,
imefikwa na msiba mwingine Mkubwa wa Msanii wa Filamu, John Stephano
Maganga aliyefariki jana katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua
kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa Mipango ya mazishi
inafanyika Nyumbani kwao Mwananyama A jirani na Kopakabana Bar jijini
Dar es Salaam.
Marehemu John
anaetarajiwa kuzikwa siku ya jumanne Makaburi ya Kinondoni Dar es
Salaam, alianza kujiingiza katika sanaa ya uigizaji mwaka 2001 chini
Thea na Deo Shija na ilipofika mwaka 2008 alianza kuigiza filamu na hadi
mauti yanamfika alikuwa njiani kutoa Filamu yake.
Aidha Wasanii wote
wanataarifiwa kufika katika Kikao Maalum Nyumbani kwa John Stephan oleo
Saa tisa alasiri kwaajili ya kupanga mikakati, ya mazishi.
Pia Mtanzania yeyote
atakae guswa na Msiba huu anaweza kutuma Rambi Rambi zake kupitia Namba
ya Tigo Pesa za 0715541714 au 0718951355
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment