 |
Lord Eyez (kulia) akiwa na wakili wake
|
Mweusi toka A- City, Lord Eyez amekutana
na waandishi wa
habari akiwa na wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa
vifaa
vya gari ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa zilizopita.Lord eyez amesema yeye kwa sasa
anaiachia mahakama ambayo
ndiyo itaweza kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama
hakuhusika
katika wizi huo wa vifaa vya gari.
Wakili wa msanii huyo anayejulikana kwa
jina la Peter
Kibatala amesema kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye
ndiye
mhusika wa wizi wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza
mahakama
ndiyo itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.Hizi kauli za mweusi huyu na wakili wake
zinaonekana
zimepimwa na ruler ya kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi
ambayo
iko mahakamani (commenting on a pending case).Weusi nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma
zinazomkabili member
huyo na kwamba tukio hili limewaathili hasa pale wanapokutana na watu
mbalimbali
na kusikia story toka kwa watu kwamba wote watakuwa wanahusika katika
tukio
hilo wakati ni story ambazo sio za kweli.Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa katika
mahakama ya mwanzo
jijini Dar es Salaam tarehe 13, 14 na 15 mwezi huu wa Novemba.
Hata hivyo the N2N soldier amesema kwa
sasa anachotaka
kufanya ni kudondonsha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya
‘surprise’
kwa mashabiki wake katika industry ya muziki wa Bongo.Lord eyez alituhumiwa na msanii mwenzake
Ommy Dimpoz kuwa
alishirikiana na wenzake kumuibia vifaa vya gari lake na tuhuma hizo
nzito
ambazo ni pigo kwa kundi la weusi kiujumla zilipelekea Lord Eyez
kukamatwa na
kushikiliwa kwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa na baadae kufunguliwa
kesi
mahakamani ambapo alipewa dhamana.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment