MWIGIZAJI
Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Yvonne Cherryl Monalisa
amewashutumu wasanii wenzake kwa kusema uongo katika jamii kuhusu maisha
yao halisi pamoja na malipo wanayopata.
Binti
huyo amedai kwa kufanya hivyo wasanii wengi wemejikuta katika maisha ya
kuunga unga kutokana uongo huo.
Baadhi ya
wasanii wa filamu wanadanganya sana kuhusu hali halisi ya maisha yao,
mtu akipata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari kuhusu malipo na
maisha yake halisi utakuta akisema kuwa yeye bila kulipwa milioni tano
hawezi kushiriki katika filamu, lakini ukweli hakuna msanii wa kawaida
anayelipwa fedha kama hizo katika tasnia ya filamu Bongo mimi mwenyewe
ni mtayarishaji, anasema Monalisa.
Anaendelea
kudai kuwa kutokana na udanganyifu huo Serikali kupitia Bodi ya Filamu
iliamua kuongeza gharama za kibali cha kurekodi filamu hadi kufikia
Shilingi 500,000 jambo lilofanya wasanii walalamike kama ni fedha kubwa
sana kulingana na malipo ya filamu, lakini ilitokana na udanganyifu
kutoka kwa baadhi ya wasanii wa filamu kudanganya, mwanadada huyo
anasema hali ya soko la filamu ni mbaya kwa sasa.
Chanzo: J2wisdom blog

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment