BOSI wa kruu ya Mkubwa na Wanaye na TMK Wanaume Family, Said Fela
‘Mkubwa’ amefungukia ishu ya Dogo Aslay kuandikwa uraia wake kuwa ni
Mkenya kwenye Tuzo za Kora 2012, Erick Evarist anashuka nayo.
Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Mkubwa Fela alisema aliyekuwa akimfanyia kampeni Dogo Aslay ili ateuliwe kuwania tuzo hizo ni DJ Tuva wa Kenya, hivyo waandaaji walijisahau na kuandika kimakosa kuwa dogo naye anatokea kwenye nchi hiyo ya Rais Mwai Kibaki.
“Kulitokea kosa la kiufundi lakini wenyewe pia wanajua kuwa Aslay ni Mtanzania, jambo la msingi ni Watanzania kumuunga mkono ili aibuke kidedea kwenye tuzo hizo ambapo wimbo wake wa Niwe Nawe unashindanishwa kwenye kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kiume Chipukizi Afrika Mashariki,” alisema Fela.

inshu iko powa
ReplyDelete