Dokta Bilal amesema mchanganuo huo ulenge pia takwimu za muda anaotumia mama kufanya shughuli za nyumbani, unyanyasaji dhidi ya wanawake pamoja na ajira kwa ujumla.
Makamu wa Rais ameelezea pia ongezeko la wabunge wanawake baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 huku akitoa changamoto kwa taasisi nyingine kuona namna ya kuwawezesha zaidi na kufikia asilimia 30 katika ngazi za maamuzi.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika Dokta Bilal amesema bado jitihada zinahitajika za kuongeza upatikanaji wa takwimu zenye mchanganuo sahihi wa kijinsia.
Takwimu za sensa ya kilimo na Mifugo ya mwaka 2008 zinaonyesha kuwa asilimia 70 ya chakula kinacholiwa na kaya binafsi hapa nchini huzalishwa na wanawake hali inayoashiria kuwa kuna umuhimu wa kumwezesha mwanamke kielimu, ajira na mahitaji muhimu katika kuendeleza uchumi wa nchi.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment