UJIO WA STAR TEN WATAKA KULETA SURA MPYA RUNZEWE

Kundi ambalo lipo kwenye maandalizi makubwa sana ya kuifanya Runzewe ionekane ni ya kisasa zaidi. Moja kati ya mambo walioandaa kwanza ni kuakikisha mji unakuwa safi hii ni pamoja na kutoa takataka zote zilizozagaa pembezoni mwa balabala pia litasimamia mambo yanayohusu mazingira ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira kupitia filamu zao watazoandaa hivi karibuni.Pia wamehaidi  kurudisha uoto wa asili ambao unaonekana kupotea katika mji Runzewe ikiwa ni kuandaa vitalu vya miti na kuvimwagilia mpaka vitakapokuwa tayari kwa kupandwa na watasambaza sehemu mbalimbali katika mji wa Runzewe kama vile hospitalini,mashuleni,misikitini,makanisani pamoja na majumbani. Maneno hayo wamesememwa na wanaSTAR TEN wenyewe walipopita mitaani kukusanya michango kwa ajili ya kuendeleza kundi lao siku chache zilizopita.

Comments

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment