Ray akiigiza kama padre
Wapenzi wa filamu za Vincent Kigosi aka Ray The Greatest wanatarajia
kufurahi mwezi huu baada ya muongozaji na muigizaji huyo kuwa mbioni
kuachia filamu mpya iitwayo ‘Sister Marry’.
Katika filamu hiyo Ray ameigiza kama padre huku Irene Uwoya akiigiza
kama mtawa ambaye alilazimishwa kuingia kwenye shughuli hiyo bila hiari
yake.
Watawa ambapo miongoni mwao yupo Irene Uwoya na
Johari wakipata maelekezo kutoka kwa mkuu wao
Johari (Sista Beata)
Akiongea kuhusiana na kisa kilichopo kwenye filamu
hiyo, mtangazaji wa East Africa Television Abdallah Ambua aka Dulla,
amesema yeye ameigiza kama Henry ambaye ni mpenzi wake na Irene Uwoya
aliyeingia kwenye utawa.
Dulla akiwa kwenye scene kushuhudia mambo
yanavyokwenda
Amesema filamu hiyo inajaribu kuonesha hali halisi ambapo masista
wengi hujikuta wakivunja amri za utawa kwa kujihusisha na vitendo viovu
ikiwa ni pamoja na kutembea na mapadre.
Ray akipitia script
Watawa
Dulla ameongeza kuwa Sister Marry inaweza kutoka mwezi huu ambapo
Blandina ‘Johari’ Chagula naye ameigiza kama mtawa anayeitwa Sista
Beata.

“Huu mzigo si mchezo subirini kwa hamu sana mara nyingi huwa sikosei
kwenye kazi zangu ni sinema niliyotumia hela nyingi sana mpaka kuona
hivi watu walivyo,” ameandika Ray kwenye blog yake.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment