Mke wa Waziri
Mkuu Mama Tunu Pinda akisubiri kula Nondozzz jana kwenye mahafali ya
Chuo Kikuu Huria Kibaha. Mama Pinda nawasihi wanawake wote wajiendeleze
bila kujali wako kwenye nafasi ipi kwani elimu haina mwisho. “Umuhimu wa
elimu hauangalii kama wewe ni mke wa kiongozi au la, elimu inawahusu
watu wote!,” alisema.
Alisema mahafali hayo yamempa hamasa ya kusoma tena zaidi na zaidi
kwani ameona wahitimu wengine wakipata shahada za juu zaidi. “Nimeona
wenzagu wakipokea Ph.D zao nikasema mimi nina Bachelor tu,
hapana. Lazima niende mbele zaidi, Mama Tunu Pinda amefuzu nakupata
shahada ya Uongozi wa biashara na biashara ya kimataifa
(BBA_INTERNATIONAL BUSINESS) katika chuo kikuu huria Tanzania ambayo
mahafali yake yamefanyika jana katika makao makuu ya yachuo hicho mkoni
pwani
Mama
Pinda akiwa na mhitimu mwingine aliyejulikana kwa jina moja tu la Flora Mama
pinda na wahitimu wenzie Mama
Pinda akipokea shada la maua toka kwa Mai Hazbendi wake Waziri Mkuu
Mizengo Pinda
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment