KIZIMBANI KWA KUCHOMA MAKANISA
![]() | ||||
| Watuhumiwawa
vurugu za Mbagala wiki iliyopita, wakiwa chini ya ulinzi wa polisi,
walipofikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza jana. Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka mbalimbali kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto wiki iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waislamu, kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. Dhamana ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30.
|
| Polisialiyejihami
kwa bunduki na radio ya mawasiliano, akishika doria kwenye lango la kuingilia chumba cha mahakama ambako watu 29 walifikishwa mahakamani hapo Jumanne Oktoba 16, 2012, wakikabiliwa na mashtaka kadhaa ya kuvamia makanisa, kuharibu, kuiba na kuchoma mali za makanisa hayo wiki iliyopita huko Mbagala jijini Dar es Salaam. Wote wamerejeshwa mahabusu hadi Oktoba 30 ambapo mahakimu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo, wameahidi kutoa uamuzi juu ya hatma ya dhamana. |



Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment