BABA mzazi wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Mzee Charles Kanumba anatengeneza tena kichwa cha habari na safari hii anadaiwa kutuma watu kuiba nyaraka za mirathi nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar.
Baba Kanumba, Mzee Charles
Kanumba.
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake, kilidai kuwa baada ya
baba Kanumba kujaribu kufungua mirathi ya mwanaye na kushindwa kutokana
na kukosa viambatanisho muhimu, amekuwa akihaha kuhakikisha anavipata
kwa njia yoyote.Kikazidi kudai kuwa hivi karibuni, mzee huyo alimpigia simu mtoto wake mmoja aishiye Dar na kumtaka ahakikishe anazipata nyaraka hizo zilizopo nyumbani kwa mama Kanumba.
“Sasa hivi baba Kanumba anahaha kweli kutafuta viambatanisho muhimu vya mwanaye ili akafungue mirathi, hii ni baada ya kwenda mahakamani kujaribu kufungua bila mafanikio kwa sababu hakuwa na ushahidi wowote kuwa Kanumba ni mwanaye,” kilidai chanzo hicho.
Marehemu
Steven Kanumba.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walifunga safari hadi
nyumbani kwa mama Kanumba ili kujua undani wa ishu hiyo ambapo bila
hiyana mama huyo alifunguka:“Ni kweli baba Kanumba alimpigia mtoto wake simu akimtaka afanye juu chini achukue nyaraka muhimu zinazomhusu Kanumba ambazo ni cheti cha kuzaliwa na hati ya kifo ili akafungue mirathi kwa sababu hivyo ndivyo vinamkwamisha.”
Hata hivyo, mama Kanumba alisema kutokana na maumivu aliyonayo kuhusu kifo cha mwanaye huyo, hana haraka ya kufungua mirathi kwani mwanaye hakuwa tajiri wala hana watoto watakaomsumbua.
Alipotafutwa baba Kanumba kuhusiana na sakata hilo,
alijibu kwa kifupi: “Aache hizo. mimi sijafanya kitu kama hicho. Kuhusu mirathi nitakutajia tarehe ya kwenda mahakamani siku ikifika.”
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment