![]() |
| DIAMOND AKATAA ZAWADI TOKA KWA WEMA |
Shoo ya “Diamonds Are Forever”, iliyochukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam usiku wa Machi 30, mwaka huu ni funga kazi ambayo kwa hakika ni namba moja kati ya nyingi zilizowahi kufanyika hapa jijini Dar.
Shoo hiyo iliyopigwa na Nasseb Abdul ‘ Diamond’ au ukipenda unaweza kumwita ‘Platinum’ ilianza majira ya saa nne usiku na kuhudhuriwa na baadhi ya mastaa wa Bongo, akiwemo mpenzi wa zamani wa Diamiond, Miss Tz mwaka 2006 na mcheza filamu,Wema Isaac Sepetu.
Diamond alidhihirisha kuwa ana jina na uwezo wa kujaza mashabiki zaidi ya elfu moja peke yake bila msaada wa msanii mwingine.
Pamoja na shoo hiyo kutawaliwa na vituko vya hapa na pale kutoka kwa Diamond na Wema bado mashabiki walipata fursa ya kufurahia na wengine kukubaliana na uwezo wa Diamond katika kulitawala jukwaa.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment