SKENDO YA USAGAJI YAMKOSESHA MCHUMBA MSANII HUYU...


MSANII ambaye amekuwa akifanya vizuri kupitia filamu mbalimbali, Edna Gabriel amekiri kuwa skendo ya usagaji iliyowahi kumtafuna huko nyuma imemharibia kiasi cha kufikia hatua ya kukimbiwa na wachumba.Edna ambaye ameigiza kwenye filamu ya Saturday Morning,  alisema kuwa tangu kuripotiwa kwa habari hiyo kila mwanaume amekuwa akimchukulia tofauti hali inayomuumiza sana.
“Yaani mpaka leo najuta na naumizwa sana na ile skendo kwani imenitibulia sana maisha yangu ya kimapenzi, wanaume sasa hivi wananichukulia kuwa mimi ‘siyo’, nakosa amani kabisa,” alisema msanii huyo.
Akasema kuwa, anachokifanya sasa ni kujisafisha kwani anatamani naye kuingia katika maisha ya ndoa kama wanawake wengine.   

Comments