
Jana Soudy Brown kapiga stori na binti aliyedai kuwa Dogo Aslay alimwambia aje Dar ili wakutane na kuweza kumsaidia kupata kazi.
Leo Said Fella kasikika na kusema hao ni matapeli waliotumia jina la Dogo Aslay na ni vizuri watu wakawa makini na mitandao ya kijamii kwa kuwa watu wamekuwa wakitumia majina ya wasanii kufanya utapeli.
Amesema huyo si Dogo Aslay wa kweli bali ni mtu aliyetumia jina lake… Soudy Brown akaona amtafute tena yule dada toka Geita ambae aliongopewa na Aslay feki mtandaoni, kajitahidi kumwambia kwamba yule hakuwa Aslay lakini dada hata hakuelewa somo.. anaamini yule alikuwa Aslay na kwa sasa yuko South Africa.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment