Diamond Platnumz ambaye ameonesha kuwa na shauku kubwa ya kuwa baba, amesema kuwa mpenzi wake Zari yupo Tanzania kwasababu zimebaki wiki chache kabla hajajifungua.
Akizungumza kwenye exclusive Interview ya Mambo Mseto na Willy M.
Tuva wa Radio Citizen ya Kenya, Diamond amesema kuwa anataka mtoto wake
azaliwe nyumbani Tanzania.
Diamond na Zari ambao wanatarajia mtoto wa kike, kila mmoja alikuwa
ana jina ambalo angependa kumuita mtoto wake, Zari anataka wamuite mtoto
wao Zara huku Diamond naye anataka amuite Candy, lakini mwisho wa siku
Diamond amesema kuwa wamekubaliana watafute jina litakalokuwa katikati
lakini lenye maadili ya dini ya Kiislam.
Katika hatua nyingine Diamond amedai kuwa awali alikuwa amepanga
kumshirikisha rapper wa Marekani Ludacris kwenye wimbo wake Nana.
Akiongea kwenye kipindi hicho, muimbaji huyo amesema kutokana na aina
ya mdundo uliotumika kwenye Nana, waliona rapper huyo wa ‘How Low’
asingeweza kufit na ndio maana aliamua kufanya na Flavour.
Amedai kuwa mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni kabisa mwa mwaka ujao,
anaweza kuachia collabo inayosubiriwa na msanii wa Marekani.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment