Mrembo na mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ , ambae kwa sasa ameamua kupiga kitabu , anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar.
Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma
na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa
akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake
mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.
“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine.
Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.
“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda
kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na
kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama supastaa.
Kwa kifupi unaweza sema Lulu amekuwa mtamu kama Mcharo!!

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment