Serikali
imesema maafisa watendaji wa vijiji na mitaa wanapaswa kijiendeleza
hadi kufikia elimu ya Astashahada kwa watendaji wa vijiji na mitaa na
kwa watendaji wa kata ni stashahada ama shahada.
Pia
imeagizwa kwamba wale wote ambao hawajafikia kiwango hicho watakuwa
wamejiondoa wenyewe katika utumishi wa uma wa ngazi hizo.
Hayo
yamesemwa bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI Aggrey Mwanry wakati akijibu swali la mbunge wa Ngara Mh
Deogratius Ntukamanzina aliyetaka kufahamu muda ambao serikali
itawaondoa watendaji wenye uwezo mdogo na kuajiri vijana wenye elimu
husika, kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya utumishi wa umma namba moja
ya mwaka 2013
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment