Mwandishi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda ameripoti kwamba staa wa soka kutoka Tanzania Mbwana Samatta ambaye anachezea club ya TP Mazembe, Congo DRC yuko nchini Hispania sasa hivi kwa ajili ya kufanya majaribio ya soka la kulipwa na club ya CSKA Moscow ya Russia ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo na kucheza katika michuano ya mabingwa wa Ulaya.
Samatta
alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku 3 na klabu hiyo kwenye
kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini ameongezewa wiki moja ya
ziada ili maofisa ya jopo ya ufundi la timu hiyo wapate muda wa
kumuangalia vizuri.
Katika moja ya mechi za majaribio alizoichezea CSKA, Mbwana tayari amefunga magoli mawili.

Mbali ya Samatta
kufanya vizuri katika mazoezi hayo, club hiyo kwenye ukurasa wa
Facebook imesema hawana mpango kufanya usajili wa mchezaji huyo kwa
sasa; “PFC CSKA trial for Mbwana State
Tanzanian striker Mbwana State is currently on trial with PFC CSKA.
He’s currently training with the team. “State will take part in one of
the two upcoming friendly matches,-our manager Leonid Slutsky told pfc-cska.com. -However, we will not be signing him. “#CSKAforever“

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment