Umbile la mwanadada aliyefahamika kwa jina moja la Avril kutoka Kenya
ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Mwanamuziki Nasibu Abdul
‘Diamond’, hivi karibuni lilionesha kumchengua msanii wa Bongo Fleva,
Omari Faraji ‘Ommy Dimpoz’ baada ya kutupia picha inayomuonesha
akikitolea macho kiwowowo cha demu huyo.
Ommy alifanya hivyo kupitia ukurasa wake wa Instragram baada kuiweka
picha hiyo kisha kuanza kukisifia kijungu cha Avril kiasi cha kumfanya
mmoja wa mashabiki wake atupie maoni akisema: “Unaonekana kaka wewe ni
mgonjwa wa wanawake waliofungashia, ila huyu demu mkali.”
Mbali na maoni hayo mengine yaliendelea kukichambua kiumbile kizuri
alichonacho mwanadada huyo na Ommy alipopigiwa simu ili kuulizwa
kilichomvutia kwa demu huyo na kama anataka kujiweka kwake alikuwa
akikata.


Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment