Ukubwa wa story hii ambayo jana aliizungumzia Martin Kadinda, Meneja wa Wema Sepetu imefanya mwandishi wetu kumtafuta Wema ili kuujua undani zaidi juu ya ishu hii ambayo ilichukua headlines kubwa Magaezetini na mitandaoni pia.
Kwenye Exclusive Interview, Wema Sepetu amesema haya;
“Taarifa
hii imenishtua sana maana asubuhi ya jana nimekuta kwenye gazeti
wameandika nikashangaa yaani hapa nimekaa kwa sababu muda mwingi
siendeshi mimi akaunti yangu ya twitter, anaiendesha mtu wangu wa blog
Bestizo maana nilikua nataka kutoa tamko“-- Wema Sepetu.
“Nilishasema
ukurasa huu tulishaufunga na nilishasema haiwezi kujirudia tena,
nashangaa watu wanarudi na maneno yale yale maana nimekaa kimya kwa kila
kitu ili kuepuka haya maneno“
“Hakuna
kitu ambacho namdai Diamond,hakuna siku hata moja nimefikiria kwenda
kumshtaki Diamond labda kama kungekua kuna kitu chochote,yaani labda
kungekua na ukweli wa kitu chochote siwezi kupoteza muda wangu kwenda
polisi,sijawahi kufanya kitu cha namna hii hizi taarifa zimenishtua sana“
“Sijawahi kujiunga VICOBA maana sivijui, nilikua nimekaa na mtu akanambia labda Wema
hujui hawa watu wa VICOBA wanajaribu kujitangaza kwa njia hii na
kutengeneza hii kitu kwamba VICOBA wanaweza kukopa hadi Milioni kumi…
kwanza mimi siwezi kukopa Milioni 10“– Wema Sepetu.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment