Muimbaji Hamis Baba aka H Baba
ambaye muda si mrefu na mkewe wanatarajia kupata mtoto wa pili kwenye
familia yao, leo ameamua kuandika kwenye ukurasa wake Instagram kuhusu
nini ambacho anakiona kwenye muziki wa mastaa wawili, Diamond Platnumz
na Ali Kiba.
Ujumbe huo unasomeka hivi ;‘Mie nawakubali wote kila mmoja ana ladha yake kwenye muziki wa #bongoflava chamsingi
tuwapeni Saport kwenye show ya jumamosi pale uwanjani leaders Club pia
kwenye Kazi zao#Sio kuzomea haipendezi kabisa wala Sio Upendo tulionao
watanzania #wote wanafanya Kazi nzuri kila mmoja ana mashabiki wake kelele za nini waacheni wafanye Kazi nzuri ili walitangaze taifa letu la #Tanzania nje ya tanzania uko kwenye upinzani Sio nyumbani? NAWATAKIA show NJEMA jumamoc iwe naamani mashabiki wote wa #KIBAna #dai’— @h_baba123
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment