Taarifa ikufikie kwamba baba wa Blue Ivy Carter na mume wa Beyonce, Jigga amenunua kampuni inayotengeneza Shampeni ya Armand de Brignac “Ace of Spades”.
Mapenzi ya Jay Z kwa Shampeni hiyo
hayakuanza leo, katika ngoma yake ya “On to the Next” aliyoifanya na
mkali Swizz Beatz aliwahi kuitaja Shampeni hiyo na katika kumpiga
kampani Obama kwenye uchaguzi wa 2012 alizionyesha chupa 350.
Kampuni inayozalisha mvinyo huo ghali
zaidi duniani haijasema kiasi cha fungu ambalo Jay kaweka kununua lebo
ya Shampeni hiyo, ila mkwanja aliouweka unamhalalisha kuwa mmiliki wa
Kampuni hiyo.
Jay ana utajiri wa dola mil. 520,
mkwanja ambao anaukusanya unatokana na miradi yake ya nguo, migahawa na
lebo ya muziki ya Roc Nation ambavyo vinamuweka kuwa tajiri wa tatu
mwana Hip Hop duniani.
Jay Z alishawahi kuulizwa; “.. unadhani kwanini unafanikiwa kila siku..?”Alijibu hivi; “.. Ni kwa sababu ya bahati.. Mimi ni mtu mwenye bahati..”
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment