0

DrugsHeadlines za dawa za kulevya ni miongoni mwa headlines ambazo zimekua zikitokea kwenye vyombo vya habari Tanzania kila wakati na zimekua zikitaja au kuhusisha baadhi ya watu maarufu, Wauzaji na hata watumiaji.
Headline nyingine ya leo Tanzania kuhusu dawa za kulevya imetokea Bungeni Dodoma ambapo Waziri William Lukuvi aliwasha kipaza sauti baada ya maswali ya mbunge Anne Kilango Malecela.
Alianza kwa kusema ‘Baada ya Wafanyabiashara wa dawa za kulevya kukamatwa na dawa hizo, uchunguzi ukishakamilika Watuhumiwa hufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kushtakiwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria, dawa za kulevya zilizokamatwa huifadhiwa na kutumika Mahakamani kama vielelezo na baada ya kesi kukamilika dawa hizo huaribiwa au kuteketezwa kwa amri ya Mahakama’
‘Uteketezaji wa dawa za kulevya umewahi kufanyika mwaka 2012  ambapo kilo tisini na mbili (92) za Heroine ziliteketezwa katika kiwanda cha Saruji Tanga kwa amri ya Mahakama na mwaka 2013 kilo mia nne kumi na mbili za bangi na kumi na mbili za Heroine, kilo tano nukta sita za Cocaine ziliteketezwa kwenye kiwanda cha Saruji Wazo Hill Dar es salaam’
Lukuvi‘Zile kesi ambazo zimechukua miaka mitatu au minne hazijaisha Mahakamani dawa zao za kulevya tunazitunza na ndio maana mwaka huu kwenye bajeti tumeomba MILIONI 300 kujenga jengo imara zaidi la kutunza dawa hizi na mmeidhinisha, kwa hiyo dawa hizi nyingi bado tunazo kwa sababu tu kesi zake hazijaisha, zinatakiwa zibaki mpaka amri ya Mahakama itakapotolewa’
Maelezo ya Waziri Lukuvi yanaendelea ambapo kwenye hii sentesi ya tatu amesema ‘zoezi la kuteketeza dawa za kulevya ni shirikishi na hufanyika chini ya usimamizi wa taasisi mbalimbali kama tume ya kuratibu udhibiti wa dawa za kulevya, jeshi la Polisi, Mahakama, ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali, baraza la taifa la usimamizi wa mazingira, Waandishi wa habari na taasisi nyingine husika
‘Serikali imeshaandaa muswada wa sheria mpya kali zaidi itakayo ondoa changamoto zilizokua zikijitokeza wakati wa matumizi ya sheria iliyokua inatumika sasa, muswada wa sheria hii mpya utawasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano huu unaoendelea’ – Lukuvi
Mahakama 1Baada ya haya maelezo ya Waziri Lukuvi, Anne Kilango alisimama na kuwasha kipaza sauti kuuliza maswali mawili ya nyongeza…. akisema ‘Kwa nini serikali inapokamata dawa za kulevya isichukue utaratibu wa kupeleka zile kesi ndani ya siku kumi na nne na kutoa maamuzi kuliko sasa zinavyochukua muda mrefu na kutoa mwanya wa hujuma ambazo Wananchi wanahisi
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu William Lukuvi akasimama na kujibu kwa kusema ‘kwa niaba ya Mh. Waziri Mkuu, ni kweli sheria hii inayotumika sasa ina upungufu mkubwa na kesi zinachukua muda mrefu sana ikilinganishwa na nchi za wenzetu kama Bangladesh, sijakwenda lakini nimesoma kwamba kwenye viwanja vyao vya ndege wameweka hata vituo na hakimu wa zamu anakuwepo palepale Airport, akikamatwa mtu anaitwa hakimu wa zamu anatoa hukumu kazi inaisha’
‘Kwa sheria yetu hii hata ukimuona mtu na dawa za kulevya haitoshi mpaka ziende kwa Mkemia mkuu alafu upelelezi ufanyike, tunazo baadhi ya hukumu mbalimbali zimetolewa vibaya pengine kutokana na sheria iliyopo, matatizo tuliyonayo yote ni kwa sababu ya sheria hii’

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X