Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi
dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore,
Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais
Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu
ya aina hiyo. Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha
saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya
Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea
kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Prof. Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya Johns Hopkins
na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi(kulia) baada ya kuwasili
katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, Marekani
kwa upasuaji Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja
na nusu ulifanyika salama.
Rais
Prof.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji
Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji
uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland
Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na
nusu ulifanyika salama.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
DAR ES SALAAM,
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment