0



UCHAGUZI wa kumpata Katibu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya jana uligubikwa na mizingwe baada ya fomu ya mmoja wawa wagombea Fanuel Mkisi kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Taarifa ya kupotea kwa fomu hiyo ilitolewa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mbeya  Joseph China, kuwa mgombea aliwasilisha fomu yake lakini wakati wakiiandaa fomu hiyo haukuoneka.
Aidha kutokana na changamoto hiyo Mwenyekiti huyo aliwatka wajumbe kuendele na uchaguzi  kwani ya jina la mgombea huyo lilisha kuwepo katika orodha ya wanaowania nafasi hiyo.
 “Ndugu wajumbe, kunasuala limejitokeza hapa na ni la ajabu, fomu moja ya mgombea haionekani na hatujui ipo wapi ila jina la mgombea tunalo,”alisema.
Kabla ya kutoa uamuzi huo Mwenyekiti huyo alimwita mgombea kwa lengo la kutaka kufahamu  fomu hiyo aliikabidhi kwa nani? ndipo Mkisi alipoeleza kuwa  kwamba fomu hiyo alimkabidhi kiongozi red Briget Jamali Juma na kwamba sababu za kufanya hivyo ni kutokana na Mwenyekiti aliyepaswa kuzipokea fomu hizo kuwa na mazungumzo na mmoja wa mgombea mwenza.
Mara baada ya Jamali kueleza hivyo danadana ziliendelea ambapo jamali alidai kuwa fomu hiyo alimkabidhi Lydia Mwaipaja ambaye naye alikiri kupokea fomu na kasha kuikabidhi meza kuu.
Kutokana na hatua hiyo baadhi ya wajumbe walilaani kitendo hicho na wengine kuwatuhumu baadhi ya viongozi kuhusika na tukio hilo, lengo likiwa ni kumbeba mgombea huyo kwa kumtafutia kura za huruma kutoka kwa wajumbe hao.
Kitendo cha kushangaza zaidi ni pale uchaguzi ulipomalizika na Mwenyekiti China,  kukutana na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa fomu ya mgombea huyo imepatikana na kwamba ilikuwa imejichanganya na makaratasi mengine yaliyokuwa kwenye meza kuu.
Kutokana na tukio kuliibuka mjadala mkali jinsi ya kuenendlea na uchaguzi amapo baadaye wajumbe warikubalian kwa kauli moja kuendlea na kwamba mgombea huyo atajaza fomu mara bada ya kufanyika uchaguzi.
Katika uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa "King Leaders Hotel" uliopo ndani ya Kata ya Nsalaga- Uyole  Jijini Mbeya ambapo mchuano ulikuwa baina ya wagombea watatu Boyid Mwabulanga aliyekuwa akiitetea nafasi hiyo Fanuel Mkisi  pamoja na Jidawaya Kazamoyo.
Kutokana mchuano kuwa mkali uchaguzi huo ulifanyika kwa awamu mbili kutokana na matokeo ya awamu ya kwanza ya wagombea wawili kugongana kwa kupata kura 14 huku mgombea watatu ambaye ni Jidawaya akipata kura 12 kati ya 41 zilizopigwa huku kura moja ikiharibika.
Msimamizi wa uchaguzi,Janson Gwilugumo ambaye ni Mwenyekiti Chadema ni msingi Kanda ya Nyanda za Juu kusini, aliomba muongozo kutoka kwa wajumbe baada ya matokeo hayo kutokidhi vigezo vya uchaguzi kwa kutofikisha asilimia 50 kama Katiba inavyoelekeza.
Baada ya kupendekeza ombi hilo, baadhi ya wajumbe walipendekeza kufanyika duru la pili kwa wagombea hao wawili kwani lengo ni kufikia asilimia 50 inayotakiwa na Chadema.
Akichangia hoja hiyo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde, alisema kutokana na kanuni za uchaguzi ni lazima kwa wagombea hao kurudia kupigiwa kura ili apatikane mshindi wa kwanza.
“Katiba ya chadema cheti ipo wazi na imeelekeza bayana kwamba  mshindi ni lazima avuke asilimia 50 hivyo kwa matokeo haya ni lazima kupiga kura kwa mara ya pili na hili halina mjadala,”alisema. Silinde
Mapendekezo hayo yaliungwa mkono na wajumbe wa baraza la mashauriano na hatimaye uchaguzi ulifanyika kwa mara ya pili na mgombea  Mwabulanga aliibuka mshindi kwa kupata kura 21 dhidi ya19 alizopata Mkisi kati ya kura 40 zilizopigwa baada ya mpiga kura mmoja kuomba udhuru.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X