Bwana Makoye Kaboje, 42 akiwa na mkewe Neema Kiwelu, 31 baada ya kunaswa.
Watu wanne wa familia moja, Makoye Kaboje, 42 (baba), Neema Kiwelu, 31
(mke) na watoto wao wawili (majina yapo) walikutwa wakilima shamba huku
wakiwa watupu! Nyakati za saa 12 alfajiri katika shamba la familia huku
wakiwa uchi.
Tukio hilo la aina yake lilijiri alfajiri ya saa 12, Septemba 2,
mwaka huu katika Kijiji cha Bushingwana Kata ya Kalemila Wilaya ya
Busega mkoani Simiyu.
Tukio hilo ambalo mpaka sasa bado gumzo, liliwashangaza wengi wakidai
kuwa ni mara ya kwanza kusikika katika mkoa huo mpya.Baadhi ya wakazi
wa kijiji hicho wanaamini si mara ya kwanza kwa watuhumiwa hao kulima
wakiwa hawana nguo, bali siku ya tukio walichelewa hadi jua linachomoza
ndiyo maana walinaswa.
“Unajua wale wana kawaida ya kulima alfajiri ili jua likitoka
wanaacha kwa kuvaa nguo na kuendelea kawaida. Sasa siku ile walijikuta
wamepitiwa mpaka jua linachomoza wao bado, ndiyo maana walibambwa,”
alisema mkazi mmoja bila kutaja jina.
Uwazi lilipofanya mawasiliano na vyombo vya ulinzi na usalama hususan
jeshi la polisi, lilikutana na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,
ACP Venance Kimario ambapo alifungukia kila kitu.
Msikie Kamanda Kimario: “Baada ya kukamatwa wakilima watupu shambani,
walifikishwa kituoni kwa ajili ya mahojiano ambapo tulibaini kuwa, wote
walikuwa wa familia moja na walikuwa wanaongozwa na baba yao.
“Walisema kulima bila nguo ni mbinu mpya ambayo walipewa na ndugu yao
mganga wa jadi kwa kuwa kufanya hivyo kutaongeza mazao, lakini hata
hivyo, mganga huyo alifariki dunia mwaka jana kwa maradhi.”
Kaimu Kamanda Kimario alisema watuhumiwa wanashikiliwa katika
Mahabusu ya Magu mkoani Mwanza kwa madai ya kufanya ushirikina
hadharani.
CREDITS:UWAZI
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment