MAAJABU!
Paka watatu wenye macho mekundu walimshangaza Kamanda wa Polisi Kikosi
cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey
Nzowa pale alipowakuta katika mlango wa ofisi yake na kumng’ang’ania
miguuni.
Akizungumza na Uwazi, askari mmoja alisema Kamanda Nzowa amekuwa
akipata vitisho na majaribu ya kila aina ikiwemo rushwa lakini kwa kuwa
ni mcha Mungu mzuri anashinda.
Hadi wageni hao wanaondoka paka hao bado walikuwa wamemng’ang’ania kamanda huyo.
Hata hivyo, kamanda huyo alirudi nyuma na kufunga mlango na kuwaacha paka hao wakiwa wamesimama nje ya mlango wa ofisi yake.
Mwandishi wetu alipomuuliza Nzowa kutokana na hali hiyo alisema ni
mambo ya kawaida kwake na kinachomsaidia ni Mungu kwani kila mara
amekuwa akisali.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment