Msanii wa muziki, Khalid Ramadhani maarufu kama ‘Tunda Man’, amedai kuwa hajawahi kuonja penzi la Wema Sepetu na wala hana mpango huo.
Akizungumza na Global TV, Tunda amesema haendani na Wema.
“Hamna kitu kama hicho, mimi kama kapteni wa Bongo FlAVA sijawahi
kulionja hilo penzi. Ni mshikaji wangu tu, kweli kabisa ni mshikaji
wangu tu ambaye ‘mambo poa’, ‘post hii picha’ napost.
"Kuna kipindi
alikuwa karibu na sister yangu Snura tukawa karibu sana. Mimi binafsi
sitamani Sepetu awe mpenzi wangu, sitamani kabisa yaani kwa sababu
nahisi kuna vitu tutakuwa tunapishana.
"Mimi nikaenda kulia na yeye
akaenda kushoto na hizi ngumi tunazocheza ninaweza piga mpaka nikaua.
Mimi najua Sepetu ni shemeji yangu najua namrespect kama shemeji yangu,”
alisema Tunda.
Pia katika hatua nyingine Tunda amekanusha kuwa na mahusiano na msanii wa Kenya, Nyota Ndogo.
“Nyota Ndogo ni kama sister yangu, rafiki yangu,” alisema na kuongeza:
“Kipindi
naenda Mombasa nilikuwa na show mbili, kuna sehemu moja inaitwa Kilifi
na nyingine ni boda ya Mombasa na Moshi, kwahiyo ukisikia naenda huko
lazima nipite kwao na huwaga ananipigia simu kama utapita huku pitia hapa
uje ule nini!
B"asi tukapita pale na team yangu akatupikia tukala
tukapiga piga picha. Lakini zile picha ambazo zilikuwa zinapigwa ni
mikao ya kisanii ambayo imewachanganya watu. Hakuna lolote na kuna ngoma
yake nimefanya kwahiyo tunashare vitu kama wasanii.”
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment