Amani!
Wakati mumewe Sunday Demonte akidaiwa kuwa yuko mbioni kuhukumiwa kwenda
jela huko Dubai, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.Staa
wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini
Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Wakati anaondoka nchini hivi karibuni, Aunt alionekana kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, akiwa na mwanaume
ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, Moses Iyobo ‘Moze’.Baada ya habari
hiyo kuripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa Wikienda, Septemba
15, mwakahuu, ilidaiwa kwamba ndugu wa mumewe, Sunday hawakufurahishwa
na kitendo hicho.
Wakipata
msosi. “Tunashangaa kumuona Aunt ameambatana na mume wa mtu na huko
anakoenda pia tunasikia watakuwa wawili tu na Kassim, inatutia shaka kwa
kweli,”alisema mmoja wa ndugu wa mume kwa sharti la kutoanika jina
lake.Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo nchini Marekani, wawili hao
walitia maguu hivi
karibuni kwa mwaliko maalum wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo
Kassim alipewa nafasi mbili hivyo akaamua kumchukua Aunt.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, baada ya wawili hao kufika nchini humo, walipanga katika hoteli moja kisha kuanza kujiachia kwenye viwanja tofautitofauti wakila bata ndani ya Jiji la New York.
Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson. Baada ya mwanahabari wetu
kunasa mchapo huo, alimtafuta Aunt kupitia WhatsApp hakupatikana,
bahati nzuri Kassim alipatikana na kusema:“Tumekuja kwa mwaliko wa
ubalozi wetu, Aunt ni mshkaji wangu kwa hiyo usishangae sana nikila naye
bata,” alijibu Kassim.


Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment