0


Kajala Masanja amedai kuwa maisha yake hayajabadilika sana kama ambavyo magazeti ya udaku yamekuwa yakiandika.

Muigizaji huyo wa filamu alisema kuwa tetesi kuwa ana fedha nyingi kiasi cha kuwa na mpango wa kumwajiri Wema Sepetu ni uzushi mtupu. “Mbona maisha yangu ni ya kawaida sana,”  Amesema Kajala.
 
“Mimi naona nipo vilevile hakuna kubwa sana lililongezeka. Nafanya shughuli zangu tu. Tatizo watu wanaamini sana magazeti. Mimi sina utajiri huo wanaouzungumzia, Kajala ni yule yule,” alisisitiza.
 
Hivi karibuni Kajala alizindua filamu yake fupi iitwayo ‘Mbwa Mwitu’.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X