Ajali za barabarani duniani hutokea kila uchao, na wahitaji wa damu wanazidi kuongezeka huku idadi ya wachangia damu nayo ikizidi kushuka siku hadi siku na kuleta hatari kwa maisha ya wahitaji.
Kutokana na hali hiyo mji wa Baoji nchini China uko kwenye harakati
za uhamasishaji uchangiaji wa damu kwa mtindo wa kipekee , kampeni
ambayo imewekwa ni kwamba kama unahitaji kujiunga na chuo,ukitaka
kujifunza udereva na hata ukitaka kuoa ama kuolewa sharti uchangie damu,
kampeni ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Sharia hiyo mpya iliyotambulishwa katika jimbo la Shaanxi
mjini,itaanza kutumika rasmi wiki ijayo inawataka askari na wanachuo wa
mwaka wa kwanza kuchangia damu walau mara moja kwa mwaka .Wananchi wa
China wanaotaka kuomba leseni za udereva,wanaopokea vyeti vya uhitimu wa
mafunzo,wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza, na wale wanaofunga ndoa kwa
msajili wa ofizi za mji wa Baoji wanapaswa kuchangia damu kwa lazima
kama mchango wao kwa jamii.
Taarifa hii ilichapishwa katika mtandao na website ya mji huo wa
Baoji, lakini kampeni hii imekumbwa na changamoto ikiwemo wakaazi wa mji
huo kuhoji damu hiyo inayotakwa kwa mtindo huo wanahoji uchangiaji
ukoje na damu hiyo itatumika wapi, badala ya kuifikiria Zaidi sharia
hiyo mpya.
Katika jimbo la Pujiang liloko Zheijang wao wameichukulia tofauti
kampeni hiyo na hivyo wanaongeza alama za ziada kwa wanafunzi wa
sekondari ambao wazazi na walezi wenye utamaduni wa kuchangia damu.
Source:BBC
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment