Nabii anayetikisa kwa maono ya vitu mbalimbali Hosea Chamungu 'Mzee wa maono' ameibuka na jambo zito baada ya kufunga kwa siku tatu mfululizo huku akifanya maombi nyikani......
Akiongea
na mwanahabari wetu mapema wiki hii, nabii Chamungu alisema
kuwa amekuwa na desturi ya kufunga siku tatu kila wiki ili
kupata maono ya mambo mbalimbali yanayojiri hapa duniani.....
Chamungu
ambaye kabla ya unabii amewahi kuwa mwanachama wa Freemasons
amesema alichofunuliwa hivi majuzi ni kwamba bado vifo
vitaendelea kuwaandama wasanii mbalimbali na kabla ya kumalizika
kwa mwaka huu wa 2014 kuna msanii mkubwa wa mziki wa Bongo
Fleva atafia jukwaani.....
"Atafariki
kwa ajili ya pesa na itakuwa jukwaani, yawezekana akawa
anagombea pesa au anatunzwa pesa jukwaani ndipo umauti
utakapomkuta," alisema Chamungu huku akisisitiza kuwa hayo ni maono na si hadithi.
Chamungu
alifafanua kuwa vifo vinavyohusisha pesa hutokana na shetani
ambao ni jamii ya Lucifer na Illuminati ambapo pia hujulikana
kama Freemasons....
"Kifo
chake kitavuta hisia za watu wengi wakiwemo wakawaida na
maarufu kama ilivyotokea kwa marehemu Kanumba lakini hatazikwa
na watu wengi kama alivyozikwa Kanumba," alisema

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment