
Payson Ariz, mtoto wa kiume wa miaka mitatu amemuua mdogo wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kwa kumpiga risasi.
Mtoto huyo alimuua mwenzake baada ya kukuta mfuko wa silaha hiyo
katika chumba cha jirani na kwenda nao katika chumba kingine kabla ya
kumfyatulia risasi mdogo wake.
Mkuu wa Polisi wa Jimbo la Arizona, Don Engler alisema uchunguzi wa
idara yake kuhusu tukio hilo lililotokea Jumanne wiki hii, utachukua
wiki moja, huku matokeo yakipelekwa katika ofisi ya mwanasheria iwapo
kukiwa na mashtaka yoyote.
“Kitakachoangaliwa zaidi ni kuhusu utunzaji silaha kwa usalama zaidi
na namna watoto hao walivyoweza kuibeba silaha hiyo ikilinganishwa na
uzito wake, sisi tunaendelea na uchunguzi wetu,” Don aliliambia Shirika
la Habari la Associated Press.
Alisema kuwa ni mapema kueleza mapendekezo ya idara yake, lakini anapisha uchunguzi ufanye kazi yake.
Wavulana hao pamoja na mama yao walikuwa wamemtembelea jirani yao
mwenye umri wa miaka 78 katika jengo analoishi, kabla ya mlio wa risasi
kusikika kwenye chumba cha kulala cha mzee huyo. Mtoto aliyempiga
mwenzake risasi alikutwa akiwa ameshikilia bastola hiyo, huku akiendelea
kushangaa kilichotokea
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment