Inauma sana! Zikiwa zimekatika
takriban siku 18 tangu alipofariki dunia aliyekuwa staa wa sinema za
Kibongo, Sheila Leo Haule ‘Recho’ (26) na mwanaye, imefahamika kuwa
mzimu wake bado unamtesa mumewe, Saguda George.
Aliyekuwa mume wa Recho (Saguda) akilia kwa uchungu wa kuondokewa na aliyekuwa mpenzi wake Recho Haule.
Nyumba
aliyopangisha Saguda na marehemu Recho Haule ambayo walilipia kodi ya
shilingi milioni tatu iliyoko maeneo ya Sinza-Kwaremy, Dar.
Habari zilieleza kwamba kabla ya
kukutwa na umauti Mei 27, mwaka huu, Recho alikuwa amepangisha nyumba
aliyokuwa anahamia kwa ajili ya malezi ya mwanaye na uzazi kwa jumla.
Ilifahamika kuwa nyumba hiyo aliilipia kodi ya zaidi ya shilingi milioni tatu ambayo ipo maeneo ya Sinza-Kwaremy, Dar.
Ilifahamika kuwa nyumba hiyo aliilipia kodi ya zaidi ya shilingi milioni tatu ambayo ipo maeneo ya Sinza-Kwaremy, Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha
kuaminika, mbali na kupangisha nyumba hiyo, pia Recho alifanya shopping
ya vitu mbalimbali vya mtoto kama nguo, midoli na vinginevyo
vinavyohitajika wakati wa kulea mtoto.
Ilisemekana kwamba Recho alivipeleka
vitu hivyo nyumbani alikokuwa akiishi na Saguda maeneo ya Kinondoni, Dar
hivyo kumpa mumewe wakati mgumu kila anapovitazama vitu hivyo.
Ilisemekana kwamba kila akivitazama vitu hivyo hulikumbuka lile jeneza dogo la mwanaye na mkewe pia na kujiona kama anaota.
Ilisemekana kwamba kila akivitazama vitu hivyo hulikumbuka lile jeneza dogo la mwanaye na mkewe pia na kujiona kama anaota.
Kuhusu nyumba aliyolipia Recho,
ilisemekana kwamba Saguda ‘ameikimbia kwani kila akienda kwenye nyumba
hiyo amekuwa akikutana na mzimu wa mkewe huyo.
Aliyekuwa mume wa Recho (Saguda) akilia kwa uchungu wa kuondokewa na aliyekuwa mpenzi wake Recho Haule.
Ilielezwa kuwa Saguda alifikia hatua
hata ya kusamehe fedha hizo (zaidi ya shilingi milioni tatu za kodi)
kwani hawezi kuishi kwenye nyumba hiyo na kwamba kama atapatikana
mpangaji mwingine bora aingie.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, tulimsaka Saguda ambaye ni bonge la cameraman na mwandishi wa miswada ya filamu za Kibongo.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, tulimsaka Saguda ambaye ni bonge la cameraman na mwandishi wa miswada ya filamu za Kibongo.
Saguda alipopatikana alisema kuwa,
baada ya kuondokewa na mpenzi wake amekuwa akiishi kwa tabu kwani kila
akitazama vitu alivyokuwa akivitumia Recho anauona mzimu wake na
kujikuta akilia.
“Hanitoki, hata nikifumba macho sura
yake hainitoki machoni. Nilimpenda sana Recho, nampenda na nitampenda
siku zote pamoja na kwamba sipo naye kibinadamu lakini kiroho tupo
pamoja kwa sababu tulipendana sana,” alisema Saguda kwa maumivu makali.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment