2
Wa kwanza kutoka kushoto aliyevaa t- shirt ya kijivu mwl Kiliba akifatiwa na mwl Ndizu, ajent Yasin, mwl Manjuu,mwl Gedi, Shaban (Shebby D) na dr Baraka
Kikundi cha Runzewe Development Group (RDG) kikiongozwa na mwenyekiti wa kundi hilo Dr Baraka na mwenyekiti msaidizi Mwl Ndizu pia muasibu wa kundi nae hakuwa nyuma Mwl Kiliba, na wengineo Mwl Manjuu na Mwl Gedi na Agenti Yasini. Walifika nyumbani hapo majira ya saa 12 jioni ya jana kwa ajili ya kumpa pole mwanachama mwenzao ndugu Shaban Dege ambaye alivamiwa na majambazi mnamo tarehe 10/04/2014 nyumbani kwake.Mwenyekiti msaidizi aliongea machache na kumwambia Shaban achukulie matatizo ni kama sehemu ya maisha kwa binadamu hivyo asikate tamaa katika utafutaji na azidi kupambana, na wengineo waliofika hapo hakuwa nyuma sana walizididi kumpa moyo sana ndugu Shaban azidi kupambna na maisha. Kiufupi Shabani nae anashukuru sana kwa moyo walioonyesha wana Runzewe Development Group, kwanza kwa kumtembelea ilo kwake ni kubwa sana imeonyesha ni jinsi gani wana upendo juu yake na wako bega kwa bega nae katika   kusukuma gurudumu lamaendeleo, Pili kwa kile walichokuja nacho pia amekipokea kwa roho safi na mungu awabariki kundi lizidi kusonga mbele zaidi.


Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X