
"Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mienendo ya mume wangu kutokana
na tabia yake kubadilika sana siku za hivi karibuni, nikabaini kuwa
kuna msichana anawasiliana naye kwa kutumiana meseji za mapenzi,
sikuwa na haraka nikaamua kufanya uchunguzi wangu kimyakimya" "Wiki
iliyopita mume wangu akiwa
amekwenda kuoga akasahau kuzima simu yake,na siyo kawaida yake kuacha simu yake bila kuizima,mara
meseji ikaingia,nikaangalia nikaona jina la mtumaji amesevu Lulu, moyo ukalipuka" Ndivyo alivyoanza kuongea mama mmoja wa makamo anayefanyakazi katika ofisi moja nyeti katikati ya
jiji la Dar alipokuja kuongea na mwandishi wetu wiki iliyopita baada ya ndoa yake kuingiliwa na mdudu
mbaya.... Akiongea kwa masikitiko makubwa, mama huyo ambaye
hakupenda kutaja jina lake kutokana na unyeti wa kazi anayoifanya,
alidai kuwa msichana huyo anayetaka kuiharibu ndoa yake yenye miaka 25
jina lake ni Elizabeth Michael.... Mama huyo alidai kuwa jina
hilo alilibaini baada ya kukuta meseji za
mapenzi kwenye simu ya mume wake na yeye kuamua kuifuatilia namba hiyo kwa kufanya kama
anataka kumtumia pesa msichana huyo na kukugundua jina
hilo.... Akiongea kwa upole, mama huyo alidai kuwa katika simu ya
mume wake, jina la mtumaji lilikuwa Lulu, lakini alipofanya uchunguzi
wake wa
kujifanya kama anatuma pesa kwa namba ya msichana huyo ndipo alipobaini
kuwa mmiliki wa namba hiyo ni Elizabeth Michael... Mwandishi alimuuliza
mama huyo kama anadhani kuwa msichana huyo
anayetaka kuiharibu ndoa yake ni muigizaji maarufu wa filamu
hapa nchini Elizabeth Michael "Lulu", lakini alikataa kuthibitisha hilo
kwa madai kuwa tangu siku hiyo namba ya binti huyo imekuwa
haipatikani.... "Baada ya kugundua siku ile , nilichukua simu yake na
kutaka kuwasiliana naye ili niweze kumuonya mwenyewe kimyakimya kwa
wakati wangu, wala sikuwa na lengo la kuja kwenye vyombi vya habari ,
lakini sikuwahi kumpata hewani tena kila nilipojaribu kumpigia"Alisema
na kuongeza:
"Huenda mume wangu alishtikia kuwa nimeona ujumbe ule, kwa sababu mimi
nilipoisoma meseji ile sikuifuta, ili akiona meseji imesomwa aelewe
nimeshajua kila kitu, pengine ndiye aliyemwambia binti huyo abadili
namba yake" Mwandishi alimuomba mama huyo ampatie namba ya huyo msichana
ili
kuweza kujua kama ni Lulu muigizaji ama siyo ( mwandishi anazijua namba
zote za Lulu ), lakini namba hiyo ni tofauti na anazotumia Lulu
Mwenyewe.... Mwandishi alipojaribu kama kumtumia pesa msichana huyo,
jina
lililotokeza ni Elizabeth Michael, na alipojaribu kuipiga namba
hiyo ilikuwa haipatikani hewani.... Juhudi za kumsaka Lulu ili
kuona kama anaitambua namba hiyo hazikuzaa matunda kutokana na namba
zake mbili kutopatikana na nyingine ikiita bila kupokelewa....
Angalizo:
Baadhi ya wasichana wa mjini wamekuwa wakitumia majina ya wasanii maarufu katika nyendo zao
ili kuwatapeli watu. Miongoni mwa njia wanazotumia ni pamoja na kujisajili kwenye mitandao ya kijamii kwa majina ya watu
maarufu ili kuwatapeli watu.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment