0


Kwa mujibu wa taarifa ya habari ilyosomwa TBC saa moja asubuhi ya Aprili 7, 2014, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo  la Chalinze, Samuel Sarianga amemtangaza aliyekuwa mgombea wa kiti cha Ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Ridhiwani Jakaya Kikwete kuwa ndiye mshindi. Mgombea huyo amepata jumla ya kura 20,828 (86.8%).

Washiriki wengine na kura walizopata ni CHADEMA 2,544 (10.5%) CUF kura 476 (1.9%) AFP 0.25% na NRA 0.25%
 
Hadi msimamizi wa uchaguzi huo alipotangaza matokeo, waliotia saini fomu ya matokeo hayo kati ya vyama vyote vilivyoshiriki ni CCM na NRA pekee.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X