Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa siku zote hawezi kudumu katika penzi la siri.
Penny
alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la Ijumaa kuainisha
kuwa tangu amwagane na Diamond (Nasibu Abdul) ambaye kila mtu alikuwa
anamjua, bado hajabahatika kuwa na mtu mwingine.
“Bado
nipo nipo sana na kama ujuavyo, mimi siwezi kuyaficha mapenzi kama
nimepata mpenzi wala haichukui muda kila mtu atajua tu,” alisema Penny.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment