CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza mkakati mpya wa kupiga
kambi katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kikidai wananchi wake
wametelekezwa kwa makusudi na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkakati huo
utawashirikisha wabunge na makada wa chama hicho ili kuwaunganisha na
kuwaamsha wananchi wa mikoa hiyo, kikidai kuwa wamesahaulika
kimaendeleo.
Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, aliyasema hayo katika mikutano ya
hitimisho ya ziara ya Operesheni M4C Pamoja Daima, ambayo ilifanyika
mkoani Pwani, juzi.
Akiwahutubia
wananchi wa mji wa Kibiti, Mbowe alionyesha kushangazwa na wananchi hao
kuendelea kubaki maskini kwa miaka yote licha ya kuwa na rasilimali
nyingi ikiwemo bahari ya Hindi.
Alisema
CHADEMA haikutilia mkazo wa kisiasa katika mikoa hiyo kwa makusudi na
badala yake iliwaachia wenzao wa Chama cha Wananchi (CUF) ambacho
kilitangulia kuweka nguvu na kuaminika katika mikoa hiyo.
Alisema
baadhi ya mikoa hiyo imebaki nyuma sana katika sekta ya elimu, jambo
ambalo alidai limefanywa makusudi na Serikali ya CCM kwa lengo la
kuendelea kuwatumia wananchi kukipa ridhaa chama hicho kutawala miaka
yote.
“Sasa nasema
haki ya Mungu tunakuja kuweka kambi mara tu baada ya Bunge la Katiba
kumalizika. Tutakuja na wabunge wetu wote, tutaweka kambi mkoa kwa mkoa,
wilaya kwa wilaya, kata kwa kata, kijiji kwa kijiji mpaka kieleweke.
“Mmetumika sana kuibeba CCM kwa kupandikiziwa ukabila na udini, sasa ifike mwisho,” alisema.
Mbowe
aliongeza kuwa Serikali ya CCM kwa makusudi imewafungia wananchi wa
mikoa ya Lindi na Mtwara kupata elimu kupitia mikutano ya kisiasa kwa
mwaka mmoja sasa ikihofia wataamshwa kuhusu rasilimali zao wanazodai
ziwanufaishe.
“Leo ni
mwaka mmoja na siku kadhaa tangu Serikali ya CCM ilipofunga mikutano ya
kisiasa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara Januari 30, mwaka jana.
“Sisi
tunaamini kwamba wananchi wa mikoa hii wamenyimwa fursa ya kupata elimu
mbalimbali, ikiwemo ya rasilimali yao iliyowekwa na Mungu ndani ya ardhi
yao,” aliongeza.
Alisema
wananchi wengi wa mikoa hiyo wamejengewa hofu na woga na CCM jambo
ambalo limewafanya wachukie wananchi wa mikoa mingine kwa kuwabagua kwa
ukabila na udini.
“Mmenyimwa
elimu bora kwa makusudi, na hii ndiyo imewafanya muwachukie makabila
mengine wakiwemo Wachaga kwa sababu tu wameendelea kielimu, wanaume
mmejengewa woga, mnatakiwa mjifunze kutoka kwao badala ya kuwachukia,”
alionya.
Makamu
Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Said Mohamed Issa, akihutubia mjini
Kibaha juzi, aliwatahadharisha wananchi wa mikoa ya ukanda huo
kutoendelea kutumiwa na CCM kupitia udini, dhana ambayo imewagawa kwa
miaka yote tangu uhuru.
Akitoa mfano
kwa wananchi wa mikoa hiyo walipoisaliti CUF wakati ina nguvu pande
zote za Tanzania Bara na Visiwani wakikubali kupandikizwa chuki kuwa
chama hiki ni cha Wapemba na Waislamu.
“Tuulizeni
sisi Zanzibar, serikali yote inaongozwa na Waislamu kuanzia rais, makamu
wake wawili, baraza la mawaziri na wawakilishi, lakini mpaka leo
ninapohutubia hapa, wapo masheikh wako ndani kwa zaidi ya miaka miwili
sasa, wamefungwa na hao Waislamu wenzao,” alisema.
Related Posts
LIVE UPDATE Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea
1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujalia uzi[...]
Sep 01, 2015Utafiti wa TWAWEZA Waibeba CCM.....Kama Uchaguzi Ungefanyika Leo asilimia 65% walisema Magufuli, 25% walisema Lowassa.
Taasisi ya Twaweza imetoa utafiti wake ambao inasema imefanya kwa wananchi wa Tanzania b[...]
Sep 22, 2015BREAKING NEWZZZ.....RAIS MAGUFULI AMTEUA KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA WA TANZANIA
KASSIM MAJALIWA [...]
Nov 19, 2015Kijana Afariki Dunia Baada ya Kufanya Mapenzi na Nguruwe Wilayani Ludewa
Kijana mmoja aitwaye Simon Dustan Mwanjavala maarufu kama Mwachakala (15) mkazi wa kijiji cha [...]
Nov 19, 2015Mabadiliko makubwa ya kisera kuinua wajasiriamali wadogo na wa kati
Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akifungua warsha. Mwasilishaji wa mad[...]
Sep 04, 2015UKAWA Kuzundua Kampeni Kesho Bila Dr. Slaa
MRATIBU wa Maandalizi ya Kampeni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Deogratia Muni[...]
Aug 28, 2015MAGUFULI AWAKUNA WANANCHI WA KARAGWE, APIGA PUSH UP JUKWAANI, WANANCHI WASHANGILIA
Kuonyesha kwamba yuko fiti ana anastahili kup[...]
Sep 22, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.