Inadaiwa kwamba watoto hao walirudi makwao kwa njia za ajabu na kusema walikuwa wamewekwa ndani kama misukule nyumbani kwa mganga huyo.
Watoto waliokuwa wametekwa na sangoma Ramadhani Issa.OFM wakiwa na mtandao wa kijamii wa Farijika, waliambiwa na watoto hao kwamba walichukuliwa na mganga huyo Desemba 27, mwaka jana wakiwa katika matembezi ya sikukuu.
“Mganga alitugusa na shanga vichwani na kutufanya tupoteze kumbukumbu na kumfuata kila alipokuwa akienda,” alisema Laurent.
Kama haitoshi walidai mganga alikuwa akiwalimisha na kuwachotesha michanga usiku kucha huku Salim akionesha chale alizochanjwa sehemu za magotini na kichwani.
Mtoto Salim alisema kuwa alimuona mwenzake Laurent akiruka kimiujiza jambo lililomshtua na kumfanya atoroke baada ya kumuona mganga huyo kauacha mlango wazi.
“Hata chakula (karanga na ulezi) tulikuwa tukipewa kingi, lakini tukila kidogo tu kinaisha kama vile tulikuwa tunakula na watu wengine,” alisema Salim.
Sangoma Rama akiandaa jeans yake baada ya kunaswa na OFM tayari kuelekea kituoni.
OFM na wazazi wa watoto hao pamoja na wanaharakati walifika kwa
mganga huyo wakiwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ujaluoni.Bahati mbaya mganga huyo alikuwa ametoka hadi ndugu yake alipompigia simu na kumtaka afike kilingeni baada ya kuambiwa kulikuwa na wateja.
Safari ya kuelekea kituoni.
Mganga huyo alifika kilingeni kwake ndipo OFM ikiwa pamoja na
mwenyikiti wa mtaa na wazazi wa watoto hao na Polisi Jamii, walimnasa na
kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi cha Nyamagana na kufunguliwa jalada
la uchunguzi MW/RB/07/2014 JALADA LA UCHUNGUZI.
Gheto la sangoma Rama kwa nje.
Mganga huyo alidai kwamba hakuwaiba watoto hao bali aliwachukua ili
wamsaidie kazi ya kumlisha paka wake huku akikana kuwachanja na
kuwafanyisha kazi usiku.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment