Maelfu ya abiria wamekwama katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma, na
kulazimika kusitisha safari zao, baada ya mvua kubwa zilizonyesha
usiku wa kuamkia siku ya Jumatano, kusababisha mafuriko makubwa
yaliyofanya daraja la Magole, linalokatiza mto kikundi katika eneo la
Dumila,kwenye barabara hiyo kukatika.
Mwandishi wetu ameshuhudia maji mengi yakiwa yameziba barabara
kuu ya Morogoro-Dodoma, huku visiki vya miti vikiwa vimeziba barabara,
na eneo la mto Kikundi unaomwaga maji mto wami, ukiwa umefurika na
daraja la magole likiwa limebomoka kabisa na kusababisha watu kutoka
upande mmoja kushindwa kuvuka kwenda upande mwingine,huku wananchi wa
eneo hilo wakidai hii ni mara ya kwanza kwa mafuriko ya aina hiyo
kutokea, yaliyosababisha mashamba na makazi ya watu kuharibika na hata
daraja kubomoka.
Wananchi hao wameshauri wakala wa barabara nchini
tanroads kuzingatia ubora katika ujenzi wa barabara na madaraja, huku
meneja wa wakala huo mkoa wa Morogoro, injinia doroth mtenga,
akizungumzia athari za uharibifu uliojitokeza, na naibu waziri wa
uchukuzi, dk charles tzeba aliyebainisha vituo 11 vya reli navyo
kuharibiwa kwa mvua,akiwashauri wananchi kukaa mbali na eneo hilo
kutokana na daraja kuzidi kubomoka kadiri muda ulivyokuwa ukiendelea
sambamba na magari kutumia njia nyingine mbadala kuendelea na safari.
Baadhi ya wananchi wameiomba serikali kufanya
jitihada za haraka, kuwanusuru wananchi waliokuwa mashambani na
majumbani,walioweza kujiokoa kwa kupanda juu ya miti, na juu ya paa za
nyumba,waliokuwa wamezingirwa na maji,ambapo mtendaji wa kijiji cha
magole, amesema mafuriko hayo yameathiri zaidi ya nyumba 300, ofisi za
serikali,shule na nyumba za ibada katika kijiji hicho, na mkuu wa mkoa
wa Morogoro Joel Bendera akibainisha tayari wameomba msaada wa helikopta
ya polisi kuwanusuru watu hao.
Kufuatia maafa hayo waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu sera na uratibu Mh. Wiliam Lukuvi amewataka wasafiri wote
waliokwama kurudi walikotoka na kutumia njia mbadala kwani daraja hilo
la dumila limeondoka kabisa. Amesema mafundi wa wakala wa barabara
tanroads wapo eneo la tukio kujaribu kurejesha mawasiliano kazi ambayo
inaweza kuchukua siku mbili au zaidi.
Ameshauri wanofanya safari kwenda Dodoma kupitia iringa au Arusha na wale waliokwama kurudi walikotoka.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment