KESI
inayomkabili Padri Deogratius Makuri wa Kanisa Katoliki Jimbo la
Singida kushindwa kutoa matunzo kwa mwanawe, juzi iliahirishwa tena kwa
mara ya tatu baada ya mlalamikiwa kushindwa kufika mahakamani.
Hakimu
wa Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini Singida anayesikiliza kesi hiyo,
Ferdinand Njau alisema Padri Makuri ametuma mtu aliyedai kuwa ni dada
yake kuja kuiarifu Mahakama kuwa hataweza kutokea kutokana na kuumwa.
Hata
hivyo, Hakimu Njau alimwambia dada huyo na wasikilizaji kwa ujumla kuwa
ili haki itendeke ni lazima mlalamikiwa awepo mahakamani. “Kuna baadhi
ya watu wanasema kwa nini labda kesi hii isingesikilizwa faragha eti
kisa tunasali naye.
“Hoja
kwamba tunasali naye haipo hapa. Ndio maana nimeamua kesi hii
isikilizwe Mahakama ya wazi. Nitasimamia kwa nguvu zangu zote
nikizingatia sheria hadi haki ipatikane maana nipo kwenye mtego.…. huyu
ni kiongozi wangu kanisani, sawa. Lakini pia huyu mtoto, malaika wa
Mungu, anahitaji matunzo. Nisipotenda haki, Mungu atanihukumu,” Hakimu
Njau alisema.
Kutokana na umuhimu huo, Hakimu Njau alisema kuwa endapo mlalamikiwa hatafika tena Januari 3, 2014, ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa, atalazimika kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.
Kutokana na umuhimu huo, Hakimu Njau alisema kuwa endapo mlalamikiwa hatafika tena Januari 3, 2014, ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa, atalazimika kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment