Kilichokua kinafata ni ndoa ambayo ilikua
imepangwa na wote wawili baada ya Linex kukamilisha hatua muhimu ambayo
ni kumvisha pete mchumba wake anaitwa Suvi raia wa Finland mwezi March
2013.
Millardayo amepata nafasi ya kuzungumza na
Linex
kwenye
exclusive interview ambayo amekiri ni kweli imebidi kila mmoja aendelee
na maisha yake na mapenzi yao kuisha kwa sababu kadhaa zilizojitokeza.
Sababu kubwa ni Suvi kutaka Linex ahamie Finland moja kwa
moja na kwenda kuanza maisha mengine kwenye hiyo nchi ambayo ndio
ingekua mara yake ya kwanza kufika, namkariri Linex akisema
‘kwa nia
nzuri kabisa imekua ngumu kwangu kukubali hayo maamuzi, nataka kuendelea
kufanya muziki wangu nyumbani’
‘Tayari nimetumia miaka zaidi ya 10
kutengeneza jina langu
kwenye muziki hapa Tanzania, bongo mimi naishi vizuri na familia yangu
naisaidia… sina tatizo la kuhangaikia maisha kwa kiasi hicho cha kwenda
kuanza tena, yani ni sawa na mtu ameshaanza chuo mwaka wa kwanza alafu
mtu anataka kukurudisha darasa la kwanza’
Sababu nyingine ni ‘mimi nimekua upande sana wa mama yangu,
tayari nimeshanunua kiwanja namjengea mama yangu na biashara pia hivyo
siwezi kuacha hii mipango isimame kwa sababu ya mapenzi, siwezi kuondoka
kwenye maisha yangu kwenda kwenye maisha mengine sababu ya mapenzi’
Linex na Suvi walikua wamepanga kuoana lakini
kwanza ilikua
Linex anatakiwa kwenda Finland kutambulishwa manake ndugu wa mke
mtarajiwa walikua wanamsikia tu hawajawahi kumuona, kisha angekwenda
Finland kufunga ndoa alafu arudi tena Tanzania kufanya sherehe kisha
aondoke moja kwa moja kuhamia Finland’
Ndoa ilikua inatakiwa kufungwa kabla ya
february 2014 ambapo
uhusiano wao umedumu kwa miaka miwili… baada ya kukutana kwa mara ya
kwanza kwenye ndege Linex akitokea Nairobi ambapo Suvi alikua anatokea
Finland na kuja Tanzania/Afrika kwa mara ya kwanza, Linex akamfanyia
ukarimu ikiwa ni pamoja na kumpeleka mpaka hotelini’
Kwa kuwa Suvi hakuwa na simu kwa wakati huo,
Linex alimwachia
namba ya simu lakini Suvi alikua kimya kwa kipindi chote cha mwezi
mmoja mpaka siku moja Linex alipokutana nae Mlimani City Dar es salaam
ndio urafiki ukaanza, Linex akawa anamtembelea hotelini na Suvi akawa
anakwenda nyumbani kwa Linex kwa kipindi cha miezi minne ndio wakaingia
mapenzini.
Credit: MillardAyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment