0
Hatimaye teknolojia imefanikisha kuwakutanisha wazazi wa mshindi wa Big Brother Afrika ‘The Chase’ Dillish Mathews baada ya mwanaume mmoja aitwaye Abdi Galgayo Guyo kuja hadharani na kudai kuwa ni baba mzazi wa mshindi huyo wa The Chase.

 Siku moja tu iliyopita, Pulse iliandika habari kuhusu mwanaume wa Kenya aitwaye Abdi Galgayo Guyo aliyetembelea ofisi za Standard Media ya Kenya na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa mshindi wa BBA Th Chase. 

Abdi ambaye kwa mujibu wa Standard ana asili ya Somalia alielezea jinsi alivyokutana na mama yake Dillish aitwaye Selma kati ya (April 1989) na (March 1990) alipoenda Namibia akiwa mmoja wa maaskari wa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini humo kusimamia amani.
  
 Habari hizo zilipokelewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali ambao wengi wao walionekana kuamini kuwa Abdi anazusha ili apate pesa, na Dillish alivunja ukimya kwa kutweet akimshangaa mwanaume huyo na kusema baba yake ana asili ya Somalia hivyo anashangazwa Abdi ametokea wapi, 

 “Why is this weird dude claiming to be my dad! My dad is Somali! Where did he fall from haaaaaaai” alitweet Dillish
 
Ubalozi wa Kenya nchini Namibia ukishirikiana na Standard Group ya Kenya jana waliandaa mkutano wa kiteknolojia kupitia ‘Google Hangout’ ili kuwakutanisha mama yake Dillish Selma Pashukeni pamoja na Abdi Guyo ambao walizungumza huku wakionana kwa mara ya kwanza baada ya kupotezana kwa miaka 23. 
  
Upande wa Namibia Selma alikuwa na mjomba wa Dillish na mkewe ambao ndio walimlea Dillish, na upande wa Kenya Abdi alikuwa mwenyewe katika ofisi za Standard Group.
   
Wakiwa wanaongea kwa furaha huku wakikumbushiana mambo yaliyotokea enzi za kukutana kwao, mama yake Dillish ambaye anaonekana bado mdogo na mrembo alithibitisha kuwa mwanaume huyo ‘Abdi’ ndiye baba mzazi wa Dillish .

Katika hali ya utani mjomba wa Dillish alimwambia Abdi akitembelea Namibia aende na pesa nyingi kufidia gharama za malezi ya Dillish. Mwisho wa mazungumzo Abdi alikaribishwa kwenda Namibia kujiunga na familia hiyo katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ambayo itakuwa September 16. 
  
 Dillish pia alithibitisha kupita twitter kwa kuandika

Tweet hiyo iliyofuatiwa na tweet nyingine “Lord, you have given me all I’ve been begging for!”

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X