Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda kwa kusaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao.
Ameeleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya
wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.
Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume
kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa
kina mama.
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake
wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke
huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi
naye.
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na
kila mmoja wao kwamba angefunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
Lakini
walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi kwa mara kwa mara lakini mwanamke
huyo alipoambiwa amchague mnmoja wao, alishindwa. Akasema anawapenda
wote wawili.
Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana
kusaini
mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama
bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa 'kwenda
kumjulia hali.'
Vile vile mkataba huo unawashurutisha
kugawana
majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na
kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.
Hata hivyo
kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume
wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku
sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment