Hatima ya msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki
wabongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa
Edward, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya kesi yao
inatarajiwa kusomwa tena tarehe 13 Agosti mwaka huu nchini humo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kikosi
cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa
wanadada hao wawili tayari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.
Alisema kuwa kutokana na ushahidi
kutokukamilika ndiyo sababu ya akinadada hao kusubiri kupanda kizimbani
tena tarehe 13 ya mwezi ujao.
Kamanda Nzowa aliweka wazi kuwa
nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo
hilo: "Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku
tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana
tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi," alisema Nzowa.
Wadada
hao ambao walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakitokea
Tanzania, walikutwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo
hazina matumizi nchini, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni
sita.
Home
»
ENTERTAINMENT
»
KITAIFA
» AGNESS MASOGANGE ATAPANDISHWA KIZIMBANI TENA TAREHE 13 AGOSTI MWAKA HUU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment