0


Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaa 5 ikiwemo SMG moja, Shortgun mbili, Riffle Mark 3 tatu, Pisto moja, Risasi 56, Maganda ya Risasi 17 na Majambazi 8.


Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Kamishna wa polisi kanda hiyo, DCP A.M. Mlege  amesema zoezi hilo lilifanyika Julai 18 mwaka huu katika maeneo ya Magomeni wilaya ya Kinondoni.


Amesema pia Jeshi hilo limeweza kukamata magari ya wizi matano, Injini tatu za magari, Vipande vya magari yaliyokatwa spea na wezi watano wa magari.


Katika hatua nyingine Jeshilo limekanusha habari zilizotolewa katika vyombo vya habari kuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika kukoswa na bomu na kumjeruhi mmoja wa wafuasi wake.


Aidha limeomba siku zingine kabla ya kutoa habari ni vizuri likaulizwa ili kuthibitisha au kukanusha.


DCO Mlege amesema pia Jeshi la polisi Kanda maalum Dar es Salaam limemkamata tapeli hatari anayetumia namba tofauti za mitandao ya simu na majina ya watu maarufu anajulikana kwa jina la Mfaume Omari maarufu kama ‘Mau’.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X