MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias
‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa
siku akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na
mashoga pamoja na watoto.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi
karibuni, Aunty Lulu alisema
kutokana na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto
waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio
One na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo
watakaojaa kwenye mazishi yake.
Alisema sababu kubwa ya msiba wake
kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla hajabadili mfumo wa maisha
anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku ya mazishi lazima wakumbuke
fadhila.
“Unajua kufa
ni kama kulala, naamini siku ya mazishi yangu
watakaokuwa wengi ni watoto pamoja na mashoga ambao zamani nilikuwa mama
yao, wengine ni waandishi na wasanii mbalimbali wa filamu na
muziki,”alisema Aunty Lulu.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment