Sio kila msanii unayemsikia kwenye radio hufanya muziki ili apate mkate wake wa kila siku. Ingawa wasanii wengi wapo kwenye muziki kwa dhumuni hilo, wapo wachache ambao hufanya kwakuwa wana kipaji na wanapenda kuimba.
Jux ni mmoja wao
Ndio maana pamoja na kwamba huzisikii sana nyimbo zake redioni, huwezi kumsikia akilalamika. Halalamiki kwasababu hana njaa. Muimbaji huyu aliyewahi kuongoza list ya Shebby D Blog ya mastaa 10 wa kiume Tanzania wanaopiga pamba kali zaidi, ameamua kuonesha jinsi ambavyo katika maisha yake hakuna vocabyurali ‘Shida’ kwa kuweka picha za noti (buruguntu) za dola za kimarekani pamoja na cheni nzito ya dhahabu.
“It’s all about my new cuban chain gold 24k I need you haters plzz dont leave me,” ameandika Jux kwenye picha hiyo.
Katika picha nyingine Jux ameonesha nguo, viatu vya brand kubwa na aghali duniani kama Versace, Gucci, Giuseppe Zanotti, Balenciaga na zingine.
Jux yupo masomoni barani Asia.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment